Sudusi

Kutoka testwiki
Pitio kulingana na tarehe 20:25, 22 Machi 2023 na imported>Kipala (Protected "Sudusi" ([Kuhariri=Zuia watumiaji wapya au wale ambao hawajajisajilisha] (bila mwisho) [Kuhamisha=Zuia watumiaji wapya au wale ambao hawajajisajilisha] (bila mwisho)))
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)
Nenda kwa urambazaji Nenda kwa kutafuta

Sudusi ni sehemu ya sita ya jumla fulani. Neno limepokelewa katika Kiswahili kutoka Kiarabu ambako linaitwa سُدْس suds. Inaweza kuandikwa pia 16 au 1/6. Ikiandikwa kwa namna ya kidesimali ni 0.166666666666667.

Katika familia ya Waislamu sudusi inataja sehemu ya urithi inayopokelewa na mama wa marehemu.

Mabaharia walitumia kifaa kinachoitwa Sudusi (ing. sextant) kwa kupima pembe za Jua na nyota baharini na hivyo wakiweza kukadiria mahali pao baharini.