Kasimwelekeo

Kutoka testwiki
Nenda kwa urambazaji Nenda kwa kutafuta

Kasimwelekeo (pia velositi[1] kutokana na Kiingereza velocity) ni kipimo cha kasi ya mwendo wa kitu kuelekea mahali fulani. [2]

Katika fizikia kasimwelekeo inataja muda unaohitajika kupeleka kitu kutoka mahali pamoja kwenda mahali pengine. Kwa hiyo ni kipimo kinachounganisha habari mbili yaani kasi na mwelekeo. Kipimo cha aina hii huitwa kipimo vekta.

Kwa mfano gari linaelekea kusini kwa kasi ya 70 km/h. Habari hizi kwa pamoja ni kasimwelekeo. <ref>Kigezo:Cite web

kasimwelekeo=uondoshajimuda + mwelekeo.[2]

Kama kitu kinazunguka kwenye duara mara moja na kufikia pale kilipotoka hakikuondoshwa. Kwa hiyo uondoshaji wake ni = sifuri na hivyo hata kasimwelekeo ni sifuri. Hii ni tofauti na kasi ya kitu kile katika mwendo wa kuzunguka.

Kasimwelekeo ni lazima iwe na mwelekeo pia.

Marejeo

Kigezo:Reflist

Viungo vya Nje

Kigezo:Commons category

Kigezo:Mbegu-fizikia

  1. Kamusi ya TUKI KKK/ESD inataja "kasimwelekeo", TUKI-KAST inataja "velositi"
  2. 2.0 2.1 Kigezo:Cite web