Namba isiyowiana
Nenda kwa urambazaji
Nenda kwa kutafuta

Namba isiyowiana (kwa Kiingereza: en:irrational number[1]) ni namba halisi ambayo haiwezi kuonyeshwa kama wianisho safi baina ya nambakamili.
Mifano mashuhuri ni kipeuo mraba cha 2 na namba ya duara π (Pi). Kwa mfano Pi ikiandikwa kwa namna ya desimali inaanza hivi 3.14159265358979 .... lakini haiwezi kamwe kuonyeshwa kikamilifu kwa kuongeza tarakimu baada ya nukta.
Tanbihi
Viungo vya nje
- Irrational Numbers, kwenye tovuti ya mathisfun.com
- Rational and Irrational Numbers, tovuti ya factmonster.com