Pembetatu mraba
Nenda kwa urambazaji
Nenda kwa kutafuta

Pembetatu mraba ni aina ya pekee ya pembetatu yenye pembe moja ya nyuzi 90°. Pembe mbili nyingine zina jumla ya nyuzi 90°.
Pande zina majina maalumu kutokana na kawaida ya wanahisabati ya Ugiriki wa Kale.
- Pande ndefu kinyume cha pembe mraba ni hipotenusi au kiegana.
- Pande mbili nyingine zinazoanza kwenye pembe mraba huitwa miguu au kwa neno la Kigiriki katheti.
| Tabia za pembetatu mraba yenye hipotenusi c | ||
|---|---|---|
| Majina ya pande | ||
| majina ya pembe | ||
| kimo | ||
| eneo | ||
| mzingo | ||
- uhakiki wa Thales husema kila pembetatu ambayo kona zake ziko kwenye nusuduara sharti ni pembetatu mraba.
- uhakiki wa Pythagoras husema ya kwaba mraba juu ya hipotenusi ni sawa na jumla ya miraba juu ya miguu (katheti).