Mjongeo

Kutoka testwiki
Pitio kulingana na tarehe 10:06, 29 Januari 2025 na ~2025-13144 (majadiliano) (André-Marie Ampère)
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)
Nenda kwa urambazaji Nenda kwa kutafuta

Mjongeo ni uwanja wa fizikia na hisabati ulioendelezwa katika umakanika kawaida, na hueleza mwendo wa nukta, gimba, na mifumo ya magimba bila kuzingatia kani zinazosababisha mwendo wake.[1][2][3][4] Fumbo la mjongeo huanza na kueleza jiometri ya mfumo na kutaja viasi vijulikanavyo kama mahali, kasimwelekeo, na mchapuko katika mfumo. Kwa hivyo kutumia kanuni za kijiometri, viasi visivyojulikana vinaweza kutatuliwa, kama vile mwendo wa baadaye wa gimba.

Mjongeo hutumika katika elimuanga ili kueleza mwendo wa violwa vya angani na makundi ya violwa hivyo. Katika uhandisi, mjongeo hutumika ili kueleza mwendo wa sehemu ziunganazo za mashine kama vile injini.

Asili ya neno

Katika Kiswahili, jina la elimu hii ni "mjongeo", kutokana na kitenzi "jongea". Istilahi hii iliundwa na wataalamu wa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili.[1] Katika lugha za Kizungu, jina hutokana na istilahi ya Kifaransa cinématique, kama ilivyoundwa na André-Marie Ampère,[5] nayo ilitokana na Kigiriki κίνημα kinema (yaani "mwendo"). Kwa hiyo, lugha za Kizungu hutumia istilahi inayofanana na ile ya Kifaransa, kama vile kinematics (Kiingereza), cinemática (Kihispania), kinematik (Kijerumani), na kadhalika.

Milinganyo ya mjongeo

Taswira 1: Jiometri ya mjongeo

Taswira 1 kijiometri inaonyesha jinsi ilivyonyambua milinganyo ya msingi wa mjongeo. Kwenye jira wima kuna kasi (v), na kwenye jira mlalo kuna muda (t). Yaani taswira inaonyesha kadiri ambayo kasi inabadilika wakati ukipita; uhusuiano huu ni mstari mwenye mwinamo, unaoonyesha kasi ikiongezeka. Mwinamo wa mstari huu ni mchapuko (a). Kijiometri, hiyo inamaanisha eneo kati ya mstari na jira la muda (eneo jekundu katika taswira) ni umbali uliosafiriwa katika muda huohuo, kwa sababu kizio cha jira la kasi ni mita kwa sekunde (m/s) na kile cha jira la muda ni sekunde (s). Hivyo, kizio cha eneo ni m/s×s, yaani m tu, iliyo kizio cha umbali.

Kuanzia hapo, umbali Δx uliosafiriwa katika muda t na kwa kasi ya kwanza v0 unatambulishwa:
Δx=v0t+12at2

Marejeo

Kigezo:Marejeo

Kigezo:Mbegu-sayansi