Mpangilio wa matendo

Kutoka testwiki
Pitio kulingana na tarehe 06:20, 9 Desemba 2024 na imported>Kisare
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)
Nenda kwa urambazaji Nenda kwa kutafuta

Katika hisabati, mpangilio wa matendo ni kundi la desturi zinazoelezea matendo yanayotekelezwa kwanza ili kuhesabu milinganyo.

Mpangilio wa matendo umesanifishwa kuliweka kila tendo katika kipaumbele maalumu. Matendo yenye kipaumbele cha juu hutekelezwa kabla ya matendo yenye kipaumbele cha chini.[1]

Vifupi

Mpangilio mara nyingi hukumbukwa kwa kifupi MAGAZIJUTO, kutokana na MAbano, GAwanya, ZIdisha, JUmlisha, TOa. Kifupi chengine ni MAPEGAZIJUTO, kutokana na MAbano, kiPEo, GAwanya, ZIdisha, JUmlisha, TOa. Hivyo, MAPEGAZIJUTO ni kamili zaidi, kwa sababu inazingatia tendo la kipeo.[1]

Mifano

Kuzidisha hukokotolewa kabla ya kujumlisha:

1+2×3=1+6=7

Matendo baina ya mabano hukokotolewa kabla ya kuzidisha:

(1+2)×3=3×3=9

Vipeo hukokotolewa kabla ya kuzidisha, na kuzidisha kabla ya kujumlisha:

1+2×34=1+3×81=1+243=244

Alama ya kipeuo, kama mabano, huweka matendo katika kundi la kukokotoa kwanza:

1+3+1×5=14×5=12×5=110=9

Mstari mlalo, alama mojawapo inayoashiria sehemu, pia huweka matendo katika kundi:

1+51+2=63=2

Marejeo

Kigezo:MarejeoKigezo:Mbegu-hisabati