Mjao

Kutoka testwiki
Nenda kwa urambazaji Nenda kwa kutafuta

Mjao (kwa Kiingereza volume) unaeleza ukubwa wa gimba la hisabati (mchemraba, tufe, mcheduara) kwa kupima nafasi ya yaliyomo yake.

Hupimwa katika vizio vya ujazo kama mita ujazo (m³) au sentimita ujazo (cm³).

Kila gimba lenye urefu, upana na kimo huwa na mjao.

Alama yake ni V.

Hali halisi ni kwamba nje ya hisabati kuna njia mbili za kuangalia mjao wa gimba:

  • ujazo wa nje kwa jumla (kwa mfano kama kitu kinazamwa katika kiowevu kinasukuma kiasi gani cha kiowevu hiki?)
  • ujazo wa ndani (kwa mfano yaliyomo ya boksi au tangi)

Mifano ya kukadiria mjao wa magimba kadhaa

Kadirio ya mjao ni Urefu x Upana x Kimo.

mchemraba mwenye urefu wa ukingo "a":
V=aaa=a3

mchemstatili mwenye urefu wa kingo "a", "b" na "c":
V=abc

tufe lenye rediasi "r"::
V=43πr3

mcheduara au mche mwenye eneo la kitako "A" na kimo "h":
V=Ah

Kigezo:Mbegu-sayansi