Uzidishaji
Nenda kwa urambazaji
Nenda kwa kutafuta

Katika hisabati, uzidishaji (kwa Kiingereza: multiplication) ni mojawapo kati ya vitendaji vinne vya hesabu(pamoja na ujumlishaji, utoaji na ugawanyaji). Uzidishaji ni kinyume cha ugawanyaji. Alama ya uzidishaji ni Kigezo:Char.[1][2]

Kwa usahihi, uzidishaji ni tendo la kujumlisha namba fulani mara kadhaa. Kwa mfano:
.
Katika mlinganyo huu, 3 ni kizidishi, 4 ni kizidishio na 12 ni zao. Kizidishi na kizidishio ni vigawo vya zao. Hata hivyo, mpangilio wa kizidishi na kizidishio haubadilishi zao. Yaani:
.
Kanuni hii hujulikana kama tabia ya mabadiliko ya kuzidisha.