Ufafanuzi mfululizo

Katika hisabati, ufafanuzi mfululizo ni mbinu ambayo huonyesha husisho kama jumla isiyokoma (au mfululizo) ya mahusisho rahisi zaidi. Ni mbinu ya kukokotoa mahusisho yasiyoweza kuonyeshwa kwa matendo ya msingi tu (ujumlishaji, utoaji, uzidishaji, na ugawanyaji).[1]
Mara nyingi, mfululizo tokeo unaweza kufupishwa hadi idadi ya vipengele vikomavyo, hivyo kutoa kadirio la husisho hilo. Kiasi vipengele vya mfululizo vinavyojumulishwa, ndivyo kadirio linavyokuwa sahihi zaidi. Mara nyingi, upungufu unaotokea kati ya kadirio na thamani halisi (yaani, jumla ya vipengele vilivyotelekezwa) unaweza kuelezwa kwa mwandiko wa O kubwa (tazama pia: ufafanuzi wa kiugo).[2]
Aina za ufafanuzi mfululizo
Mfululizo wa Taylor
Kigezo:Main Mfululizo wa Taylor ni mfululizo wa vipeo unaotokana na vinyambuo kwenye nukta moja.[3] Kihususa, kama husisho likitenguka kiusokomo kuzunguka nukta , hivyo mfululizo wa Taylor wa kuzunguka nukta hiyo watolewa na:
ikiwa desturi .[3][4] Mfululizo wa Maclaurin wa ni mfululizo wake wa Taylor kuzunguka .[5][4]
Mfululizo wa Laurent
Kigezo:Main Mfululizo wa Laurent ni jumuisho la mfululizo wa Taylor, ukiruhusu vipengele vyenye vipeo hasi; mfululizo una umbo wa na hukutana kuelekea kipete.[6] Hasa mfululizo wa Laurent unaweza kutumiwa ili kuchunguza mwenendo wa husisho changamano karibu na shani ukifikiriwa ufafanuzi mfululizo kwenye kipete chenye shani ya kitovuni.
Mfululizo wa Dirichlet
Kigezo:Main Mfululizo wa Dirichet una umbo
Mfululizo wa Fourier
Mfululizo wa Fourier ni ufafanuzi wa mahusisho ya kurudiarudia kama jumla ya sini na kosini.[7] Mfululizo wa Fourier wa husisho lenye kipindi cha watolewa na uonyesho:
ambapo vizigeu vyatolewa na fomula:[8]
Mifano
Yafuatayo ni mfululizo wa Taylor wa : [9][10]
Mfululizo wa Dirichlet wa husisho zeta la Reimann ni [11]